
Serikali kuwalipa fidia wananchi wa Igunga waliopitiwa na bomba…
Serikali imesema itahakikisha wananchi wa wilaya ya IGUNGA mkoani TABORA waliopitiwa na mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka HOIMA nchini UGANDA hadi mkoani TANGA wanalipwa fidia baada ya maeneo yao kufanyiwa tathmini.
Mkuu wa idara ya usafi na mazingira wilayani IGUNGA,FREDRICK MNAELA amesema wananchi waliopitiwa na mradi huo watalipwa fedha zao kwa wakati baada ya serikali kukamilisha tathmini ya maeneo husika.
Amesema wilaya ya IGUNGA ina kata ambazo zitanufaika na mradi wa bomba la mafuta na kwamba baadhi ya kata itajengwa kambi ya mafundi wa ujenzi wa mradi huo.
Kwa upande wake,Afisa Mtendaji wa kijiji cha BULYANG’OMBE katika kata ya NANGA,SAID KIMENYA amesema anaamini kuwa wananchi waliopo katika kijiji chake watalipwa fidia zao huku akisema kambi ya bomba ya bomba la mafuta itajengwa kwenye kijiji hicho.
Naye mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha BULYANG’OMBE,ASHA RASHIDI amesema kwamba kupita kwa bomba la mafuta kutoka nchini UGANDA hadi bandari ya TANGA ni jambo zuri huku akisema wananchi wake watapata ajira.
Aidha mwananchi ambaye bomba lake litapitiwa na mradi huo katika eneo MIHAYO SHATILA amesema kuwa vitu mali zilizofanyiwa tathimni ni mazao amabyo yapo kwenye eneo lake.
Amesema kuwa anaamini serikali itatenda haki kwa wale wananchi ambao wanatakiwa kufidiwa ili waweze kutafuta maeneo mengine.
MWANDISHI:AVELIUS EVODIUS,CGFM.