Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

ANC chazidisha shinikizo dhidi ya Zuma

  • February 6, 2018

Subira inawaishia viongozi wa chama tawala Afrika kusini ANC dhidi ya rais wa Jacob Zuma waliomtarajia kujiuzulu baada ya majadiliano ya wiki kadhaa sasa.

Hapo jana usiku viongozi wa chama cha ANC walitangaza kwamba wataitisha mkutano wa kiwango cha juu wa kamati ya kitaifa NEC kuondosha mzozo wa kisiasa kwa lazima.

Mkutano huo unaotarajiwa siku ya Jumatano unatafanyika siku moja kabla ya hotuba ya bunge ya kila mwaka anayotarajiwa kuitoa Zuma bungeni.

Matarajio ni kwamba NEC itapiga kura kumuondoa madarakani.

Lakini Zuma anaweza kwenda kinyume na matakwa ya chama. Hilo basi litaweza kuzusha uwezekano mkubwa na ambao haujawahi kufanyika wa wabunge wa ANC kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

HIzi ni siku muhimu katika demokrasi ya Afrika kusini. Amesema kuwa, wanakutana kujadili ubadilishanaji madaraka kutoka Rais Zuma kama mwenyekiti wa zamani na sasa Cyril Ramaphosa ambaye ni kiongozi mpya wa chama hicho.

Siku ya jumatatu viongozi wandamizi wa chama hicho walilazimika kuwa na mkutano wa dharula mjini Johannesburg kujadili hatima ya rais Zuma.

Hata hivyo rais Zuma ameshikilia msimamo wake kutokubaliana na shinikizo la kumtaka aachie madaraka.

Mwezi Disemba mwaka jana Ramaphosa alimrithi rais Zuma katika nafasi ya juu ya kukiongoza chama hicho kikongwe barani Afrika.

Rais Zuma amekuwaakiandamwa na kashfa za rushwa, ambapo katika miaka ya hivi karibuni alihusishwa na familia yenye asili ya India ijulikanayo kama Gupta – ambapo inadaiwa alitumia madaraka yake vibaya ili kujinufaisha yeye na washirika wake hao.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Esmond Bradley Martin: Mchunguzi jasiri aliyewakabili wawindaji haramu auawa Kenya
Wenyeviti wa serikali za vijiji na maafisa watendaji wa vijiji na wilayani UYUI wameonywa kuacha tabia ya kuchukua fedha za wananchi bila kuwapa stakabadhi.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise