Asilimia 67 ya maradhi ya tumbo yanatokana na uchafu…

Akizungumza na CG FM katika kuadhimisha siku ya kunawa mikoni, Afisa Afya Mwandamizi wa manispaa ya TABORA VEDASTUS CHEYO, amesema watu wanakosa umakini wa kunawa mikono hali inayosababisha kuugua magonjwa ya ya tumbo.
Naye Dakari JUSTINA NKOME wa Kituo cha Afya cha EPHATA katika Halmashauri ya Manispaa ya TABORA amesema wazazi watumie siku hii kuzingatia usafi kwa watoto wao ili kuzuia vifo kwa sababu watoto elfu mbili hufariki duniani kila siku kutokana na madhara ya kutonawa mikono.
Maadhimisho ya siku ya kunawa mikono duniani kwa TANZANIA husaidia kuhamasisha umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni na kukuza uelewa wa jinsi inavyosaidia katika kuokoa maisha ya watoto na jamii kwa jumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni mikono safi kwa manufaa ya sasa na ya baadaye.