Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
Entertainment

Baada ya kuzinguana na Drake kwenye video ya ‘Come…

  • March 20, 2018

Kwa mashabiki wa muziki hususani muziki wa Nigeria watakumbuka kuwa kwenye video ya ‘Come Closer’ ya  Wizkid aliyomshirikisha Drake kutoka Marekani, Msanii huyo hakuonekana kwenye kichupa hicho kitu ambacho kiliibua maswali mengi na baadhi ya mashabiki kumshambulia Wizkid.

Tokeo la picha la wizkid

Wizkid

Sasa ukweli ni kwamba ingawaje walizinguana na baadaye kuonekana kupatana ukweli ni kwamba kitendo cha Drake kutoonekana kwenye video hiyo bado kilikuwa kinamuumiza sana Wizkid mpaka leo.

Wizkid amesema kuanzia mwaka huu hata’shoot tena video yoyote ile nje ya bara la Afrika na video zote ambazo amesha’shoot nchini Marekani hataziachia.

Akizungumza kwenye mahojiano yake Jumamosi iliyopita na kituo cha Redio cha The Beat 99.9 FM cha nchini Nigeria, Wizkid amesema maamuzi hayo aliyapanga toka mwaka jana baada ya kuona hakuna umuhimu wa kupoteza hela nyingi kwa ajili ya ku’shoot video ughaibuni.

“Nimeamua kwa sasa sita’shoot tena video zangu nje ya nchi, Nataka nifanyie video zangu na kila kitu hapa hapa Afrika, Kwa hiyo hata video zangu nilizo’shoot mjini Los Angeles (Marekani) sitazitumia tena,“amesema Wizkid baada ya kuulizwa swali lililohoji kwanini kwenye albamu yake ya ‘Sound From The Other Side’ hakuna hata video moja.

Hata hivyo, taarifa hizo hazijapokelewa vizuri na mashabiki wake huku wengi wakihusisha maamuzi hayo kuwa yamekuja baada Drake mwaka jana kutoonekana kwenye video ya Come Closer.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Rais Magufuli atoa wiki moja kwa Mawaziri kushughulikia changamoto hii
Brazil: Lula da Silva kufungwa miaka 12 jela

Related articles

Mashabiki wa klabu ya YANGA…
Lagos, NIGERIA: Yemi Alade na…
STEPH CURRY aiongoza Golden State…
ShiiKANE Diamond alistahili tuzo
The Story of Adisson yaharibu…
Nicki Minaj kuachia albamu yake…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise