Baadhi ya wanasiasa katika halmashauri ya Manispaa ya TABORA…

Baadhi ya wanasiasa hao,KANANDA PAULO diwani wa kata ya MBUGANI kupitia Chama cha Mapinduzi CCM na Katibu wa Chama cha Demekrasia na Maendeleo-CHADEMA,MSABAHA KAMBAMBOVU wamesema Tume ya Uchaguzi na Mipaka nchini KENYA ingemaliza kwanza tofauti zilizopo kabla ya kufanyika uchaguzi.
Kwa upande wake,Mchambuzi wa masuala ya kisiasa EDGAR PASTORY ambaye ni Mhadhiri Msaidizi katika Chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu AGUSTINO cha AMUCTA cha mjini TABORA amesema kufanyika kwa uchaguzi nchini KENYA kwa kushirikisha wafuasi wa chama kimoja kunaweza kusababisha mpasuko nchini humo.
Mhadhiri PASTORY ameongeza kuwa serikali ya KENYA iangalie uweekano wa kurudi katika meza ya mazungumzo ili kufikia muafaka jinsi ya kumaliza mgogoro wa kisiasa uliopo nchini humo.
Mpinzani Mkuu RAILA ODINGA na Muungano wa vyama vya upinzani wa NASA wamesusia uchaguzi huo kutokana na kutokuwa na imani na Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya nchi hiyo baada ya kufutwa kwa uchaguzi uliofanyika Agosti nane mwaka huu.