
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo…
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha KOREA KASKAZINI cha kurusha kombora kupitia anga ya JAPAN huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza kitendo hicho.
Taarifa iliyotolewa na MAREKANI haikutishia kuiwekea vikwazo vipya KOREA KASKAZINI.
Lakini Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka KOREA KASKAZINI kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nyuklia.
Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka KOREA KASKAZINI kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.
Majeshi ya KOREA KUSINI na MAREKANI yamekuwa yakishiriki mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa KOREA KASKAZINI,jambo ambalo KOREA KASKAZINI inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi.