
Basi la AN Classic (MWANZA-TABORA) lalamikiwa na abiria kwa…
Abiria wanaosafiri kuelekea MPANDA wamelilalamikia Basi la AN CLASSIC linalofanya safari zake MWANZA – TABORA kuwafaulisha badala ya kuwafikisha mwisho wa safari yao kama ilivyoainishwa kwenye tiketi zao.
Wakizungumza na CG FM baada ya kushushwa ndani ya basi hilo katika stendi mpya ya mabasi mjini TABORA abiria hao wamesema kitendo hicho kimewakwaza kwani tiketi zao ni za moja kwa moja hadi MPANDA na hawakufahamishwa kuwa gari hilo halifiki huko.
Afisa mfawidhi wa Mamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini –SUMATRA Mkoa wa TABORA JOSEPH MICHAEL amekemea kitendo cha kufaulisha abiria na kuamuru basi hilo kuchukua kibali cha muda ili liwapeleke abiria hao MPANDA.