Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls yavunjwa…

  • June 6, 2018

Wizara ya Elimu nchini Kenya imeivunjilia mbali bodi ya usimamizi wa shule ya Moi Girls na kutangaza kwamba ni marufuku kuwatembelea watoto shuleni baada ya mapumziko ya katikati ya muhula kwa shule zote za upili za umma.

Hii ni kufuatia uchunguzi unaoendelea kubaini kesi ya ubakaji wa mwanafunzi katika shule hiyo.

Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed alitoa agizo kwa maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote kuepuka uwezekano wa wanafunzi kuingiliwa.

Mwalimu mkuu katika shule ya upili ya Moi Girls amewasilisha ombi kwa tume ya kuwaajiri walimu nchini TSC, kutaka kustaafu mapema baada ya kuzuka tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo mwishoni mwa juma ndani ya shule hiyo.

Walimu pamoja na wafanyakazi wengine wakiume katika shule ya upili ya Moi Girls Nairobi wametakiwa kufanyikwa uchunguzi wa DNA wakati maafisa wa upelelezi wanajaribu kuchunguza tuhuma za kubakwa kwa mwanafunzi katika shule hiyo Ijumaa usiku.

Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed
Waziri wa Elimu nchini Amina Mohammed ameagiza maafisa katika wizara yake wafanye upya ukaguzi wa usalama katika shule zote

Polisi wamewaagiza walimu hao wa kiume, walinzi na jamaa wa kiume wa walimu wanaoishi ndani ya Shule hiyo au wale wanaoaminika kuwa walikuwa ndani ya shule hiyo mapema Jumamosi asubuhi.

Uchunguzi huo wa DNA ni muhimu katika kubaini kesi za unyanyasaji wa kingono na hutumika kumithilisha mshukiwa dhidi ya maji maji yanayopatikana katika mwili wa muathiriwa na hivyo kuweza kuwana ushahidi mzito katika kesi.

Itasaidia pia kubaini iwapo washukiwa wataokaochunguzwa walikuwa katika eneo la tukio hilo la uhalifu au kuwaondoshea makosa yoyote.

Polisi wanajaribu kuchunguza matukio yaliojiri usiku huo wa mkasa na siku ya pili iliyofuata kujua ukweli upo wapi katika tuhuma hizo za kubakwa kwa wanafunzi wa Moi Girls ambazo zimezusha hasira kubwa nchini.

Maafisa wanachunguza pia tuhuma kwamba maafisa katika shule hiyo waliwaambia wanafunzi wajioshe na wanyamaze kuhusu kinachotuhumiwa kutokea.

Mambo muhimu ya kufanya kumsaidia muathiriwa wa ubakaji:

Kenya iliidhinisha sheria ya uhalifu wa kingono na muongozo wa kitaifa kuhusu namna ya kushugulikia visa vya unyanyasaji ili kutoa nafasi kwa watoto kupata huduma za afya.

Hivyo basi katika kesi hii, sheria ya Kenya iko wazi kwamba mwanafunzi aliyebakwa ana haki ya kupata huduma ya baada ya kubakwa.

Jennifer Kaberi, mtaalamu wa malezi ya watoto Nairobi anasema hatua ya kwanza kuchukua wakati mtoto anaponyanyaswa ki ngono, ni :

  • Mkimkimbize hospitali muathiriwa katika muda wa saa 72 baada ya ubakaji.
  • Piga ripoti katika kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
  • Usimuoshe au kusafisha sehemu yoyote ya mwili wa muathiriwa.
  • Usizioshe au kuziharibu nguo alizovaa muathiriwa, badala yake ziweke kwenye mfuko wa kaki na sio mfuko wa plastiki.
  • Madaktari watakagua kiwango cha majeraha na kumtibu mtoto.
  • Watampa dawa pia ya kumkinga na virusi vya HIV au kupata uja uzito.
  • Ripoti ya daktari itatumiwa katika uchunguzi wa polisi kwenye kesi.
Presentational grey line

Bi Kaberi anaongeza kwamba katika kesi nyingi za watoto kubakwa, huwa hakuna usiri wala faragha na hiyo ni kwasababu ya kusaidia maafisa wa afya kumtibu mtoto, na kuruhusu polisi wachunguze kwa kina kesi iliopo.

Vyombo vya habari nchini vinaripoti kwamba ripoti ya daktari imethibitisha kwamba msichana wa shule hiyo alibakwa.

Mkasa huu umetokea hata wakati ambapo maandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu kilichotokea.

Maandamano yamefanyika mjini Nairobi siku ya Jumatatu kulalamika kuhusu tuhuma za ubakaji katika shule ya Moi Girls NairobiWaandamanaji hao waliojumuisha wanafunzi wa zamani wa shule hiyo waliandamana nje ya shule hiyo wakiwa wamebeba mabango

Waandamanaji hao waliojumuisha wanafunzi wa zamani wa shule hiyo waliandamana nje ya shule hiyo wakiwa wamebeba mabango yaliokuwa na ujumbe wa kupinga ubakaji.

Gazeti la Daily Nation linaripoti kwamba tayari maafisa wa upelelezi kutoka kitengo cha uhalifu mkubwa na mwanakemia wa serikali hapo jana Jumatatu walichukuwa sampuli za wafanyakazi wanane wa shule hiyo miongoni mwao walimu 6 ili kufanyiwa ukaguzi wa maabara.

Kwa sasa shule hiyo imefungwa kwa wiki moja huku uchunguzi ukiendelea.

CHANZO: BBC Swahili.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu mpya kutatua mgogoro

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…
Burundi kuitambulisha katiba mpya siku…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise