Sports

Rooney ashindwa kuisaidia Everton Goodison Park.

Straika wa Everton Wayne Rooney.

Klabu ya Everton inayodhaminiwa na kampuni ya kubashiri matokeo ya SportPesa hapo jana ikiwa katika Uwanja wake wa nyumbani wa Goodison Park ilikubali kipigo kibaya cha mabao 5-2 dhidi ya Arsenal mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Waliyoihangamiza ngome ya Everton usiku wa jana walikuwa ni wachezaji,Mesut Ozil, Nacho Monreal , Alexandre Lacazette na Aaron Ramsey wakiifungia Arsenal wakati Wayne Rooney akiifungia The Toffee bao lake la kwanza wakati lapili likifungwa na Oumar Niasse.

Kwa matokeo hayo Everton mpaka sasa inakuwa imepoteza idadi ya michezo mitano wakati Arsena ikipaa kileleni hadi nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi.

Entertainment

DJ KHALED NA DIDDY WAFULULIZA PARTY KATIKA KUMBUKUMBU YA…

Dj Khaled na Mwanaye Asahd.

Mtoto wa kwanza wa kiume wa Mfalme wa mtandao wa Snapchat, Rapa, Mtangazaji na Dj ‘Dj Khaled’, Asahd Tuck Khaled tarehe ya leo ametimiza umri wa mwaka mmoja na sherehe za hatua hii ya umri zilianza siku ya Jumamosi ukumbi wa LIV nightclub unaopatikana Fountainebleu huko mjini Miami. Read more “DJ KHALED NA DIDDY WAFULULIZA PARTY KATIKA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA KWA ASAHD KHALED”