Local

Wananchi wametakiwa kuepuka matumizi ya bidhaa za vyakula na…

Wananchi wametakiwa kuepuka matumizi ya bidhaa za vyakula na dawa zilizopita  muda wake.

Wananchi wametakiwa kuepuka matumizi ya bidhaa za vyakula na dawa zilizopita  muda wake wa matumizi pamoja na vipodozi vyenye viambata sumu ili kujiepusha na madhara wanayoweza kumpata mtumiaji.

Wito huo umetolewa na Meneja wa Mamlaka ya chakula na dawa Kanda ya Magharibi Dakta EDGER MAHUNDI, katika zoezi la kuharibu bidhaa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu, tani 17.5 zenye thamani ya shilingi milioni 55.

Amesema bidhaa  hizo zimekamatwa katika mikoa ya TABORA, KIGOMA na KATAVI na kwamba mamlaka hiyo ina jukumu la kukagua maeneo yote yanayojihusisha na bidhaa wanazodhibiti kwa kushirikiana na maafisa wa afya na wafamasia.

Afisa Afya Mkuu Manispaa ya TABORA PASCHAL MATAGI amewashauri wananchi watumie bidhaa zilizoandikwa kwa lugha wanazozielewa kama vile Kingereza na Kiswahili.

Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imewasisitiza kujali afya zao, kwa kuzingatia  matumizi sahihi ya bidhaa na kuwafichua wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kwa kutumia njia za panya.

Amesema bidhaa  hizo zimekamatwa katika mikoa ya TABORA, KIGOMA na KATAVI na kwamba mamlaka hiyo ina jukumu la kukagua maeneo yote yanayojihusisha na bidhaa wanazodhibiti kwa kushirikiana na maafisa wa afya na wafamasia.

Licha ya uwezo wa kiuchumi kuwa mdogo kwa baadhi ya wananchi, Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imewasisitiza kujali afya zao, kwa kuzingatia  matumizi sahihi ya bidhaa na kuwafichua wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa kwa kutumia njia za panya.