
Daktari aelezea visababishi vya watoto kufariki tumboni.
Kupitiliza kwa mimba,magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na kifafa cha uzazi ni miongoni mwa visababishi vya watoto kufariki tumboni au mama mjamzito kujifungua mtoto mfu.
Daktari wa kitengo cha magonjwa ya wanawake afya ya uzazi na kizazi MNUBI BAGUMA katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa TABORA KITETE amebainisha visababishi vingine kuwa ni maambukizi ya virusi Malaria na Kaswende.
Amesema mama mjamzito akishika ujauzito chini ya miaka 18 na zaidi ya miaka 35 kuna uwezekano mkubwa wa kupitiliza wakati wa kujifungua na hivyo kusabisha mtoto kufariki tumboni.