Diamond Platnumz atoa povu kwa wanaofuatilia maisha yake ya…
Diamond Platnumz ameamua kutema cheche kutokana na watu kufuatilia mahusiano yake kwa ukaribu kila kukicha.
Kupitia mtandao wa Instagram, hit maker huyo wa ‘Hallelujah’ ameonekana kuumizwa na maneno yanayoendelea kuzungumzwa mitandaoni na kuamua kusema kuwa ikifika muda wa kuweka wazi atafanya hivyo kwani hakuna kitakacho mzuia.