Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Faru wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afa.

  • March 20, 2018

Sudan, faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45, shirika la Ol Pejeta limetangaza.

Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.

Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.

Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.

“Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana,” Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.

“Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wnayama cha Dvur Kralove, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake.”

Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.

Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove miaka ya 1970.

Miaka ya baadaye, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta.

Alichangia kuendeleza faru wa aina yake kwa kutungisha mimba faru wengine na kuchangia kuzaliwa kwa faru wengine wawili wa aina yake ambao sasa ndio pekee waliosalia hai.

Ujumbe wa Twitter wa @OlPejeta: Sudan will be remembered for his unusually memorable life. In the 1970s, he escaped extinction of his kind in the wild when he was moved to Dvůr Králové Zoo. Throughout his existence, he significantly contributed to survival of his species as he sired two females.

Faru hao kwa jina Najin na Fatu ni wa kike lakini ni tasa.

“Kadhalika, chembe za jeni zake zilichukuliwa na kuhifadhiwa jana kabla ya kifo chake kwa matumaini kwamba zitasaidia katika juhudi za siku za usoni za kuwazalisha faru kupitia teknolojia ya jeni na seli,” Ol Pejeta wamesema.

Ujumbe wa Twitter wa @OlPejeta: Unfortunately, Sudan’s death leaves just two female northern white rhinos on the planet; his daughter Najin and her daughter Fatu, who remain at Ol Pejeta.

Matumaini pekee sasa ya kuendeleza faru wa aina ya Northern White Rhino ni kupitia teknolojia ya kutungisha mbegu kwenye mayai ya mnyama nje ya mwili wa mnyama huyo, maarufu kama IVF.

Sudan the white rhino

Hilo linatarajiwa kufanyika kwa kutumia mayai yaliyovunwa kutoka kwa faru jike walio hai kwa sasa pamoja na mbegu za kiume kutoka kwa faru wengine wa kaskazini.

Shughuli ya kutungisha mbegu mayai hayo ikifanikiwa, basi faru wa karibu aina ya Southern White Rhino watatumiwa kubeba mimba hiyo.

Kutumiwa kwa mtandao wa Tinder

Mwaka uliopita, shirika la Ol Pejeta lilizindua kampeni ya kuchangisha pesa kupitia kufungua akaunti kwenye mtandao wa kutafuta wapenzi wa Tinder.

Lengo lilikuwa kuchangisha dola milioni 9 zitakazofadhili utafiti wa kutafuta mbinu mbadala za kutumia mbegu zao kuzalisha.

Tinder inaongoza ulimwenguni miongoni mwa mitandao ya kijamii inayotumika kutafuta marafiki na wapenzi.

Kupitia kampeni #TheMostEligibleBachelor, Tinder walitumai picha ya Sudan ingeonekana katika mataifa 190 ulimwenguni.

Kampeni hiyo ilidhaniwa kuwa njia pekee iliyosalia ya kuokoa faru hao wanaokabiliwa na hatari kubwa ya kuangamia.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Wadau wa kilimo watoa ombi kwa serikali
Trump apendekeza adhabu ya kifo dhidi ya walanguzi wa mihadarati

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise