Fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kwa shule za…

Wakuu wa shule za msingi na sekondari wametakiwa kutumia fedha za ruzuku za wanafunzi zinazotolewa na serikali kwa kuzingatia mwongozo wake.
Rafiki wa Mtandao wa Elimu TABORA,YAHYA HEMED amesema pamoja na shule nyingi kutumia fedha za ruzuku vizuri kwa mwaka wa fedha wa 2016-2017 lakini wakuu wa shule hawakuzingatia mwongozo ulio katika mtaala akitoa mfano kwa shule za msingi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Marafiki wa Elimu TABORA,EMANUELI MWAKALINGA amesema katika utafiti uliofanyika katika shule wamegundua uelewa na uwazi ni mdogo kwa wahusika.
Mbunge wa jimbo la TABORA mjini,Mheshimiwa EMMANUEL MWAKASAKA amewataka walimu wakuu na wadau wa elimu kuzingatia takwimu katika matumizi ya fedha za ruzuku ili kuleta maendeleo katika sekta ya elimu.
Baadhi ya walimu walihudhuria kikao hicho wamesema mpango huo ni mzuri lakini una changamoto zake.