Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Giggs anavutiwa na kazi Leicester na Everton.

  • October 24, 2017October 24, 2017
Ryan Giggs alichezea Manchester United mechi 963 na alikuwa msaidizi wa Louis van Gaal uwanjani Old Trafford.

Jagina wa Manchester United na Wales Ryan Giggs amesema anavutiwa na nafasi za kazi za umeneja katika klabu za Leicester na Everton zinazocheza Ligi Kuu England.

Klabu zote mbili hazina mameneja baada ya Leicester kumfuta kazi Craig Shakespeare wiki iliyopita.

Everton walimpiga kalamu Ronald Koeman Jumatatu.

Giggs alikuwa mkufunzi msaidizi wa Louis van Gaal uwanjani Old Trafford, na alisailiwa kwa kazi ya umeneja Swansea mwaka 2016.

“Kwangu, hizi ni klabu ambazo zinaweza kunivutia,” Giggs, 43, ameambia Sky Sports.

“Nafikiri ukiangalia timu hizi mbili, Leicester walikuwa mabingwa misimu miwili iliyopita, Everton nao ni klabu nzuri na yenye historia nzuri.

“Hata hivyo, kuna wakufunzi wengi huko nje ambao pia watavutiwa na nafasi hizo.”

Giggs haaminiki kuwa miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuchukua kazi ya umeneja Everton.

Leicester nao wanaonekana kuimarika chini ya kaimu meneja Michael Appleton ambapo walilaza Swansea 2-1 uwanjani Liberty Stadium.

Klabu moja ya ubashiri imeweka uwezekano wa Giggs kuwa meneja wa Chelsea kuwa 12/1, Chris Coleman naye nafasi yake 6/1 na Claude Puel ndiye anayepigiwa upatu zaidi katika 4/7.

Giggs hajajishirikisha katika soka ya kiwango cha juu tangu kufutwa kwa Van Gaal Mei 2016.

Aliondoka katika klabu hiyo Julai 2016 na akaanza mapumziko ingawa amekuwa akisisitiza kwamba anakusudia baadaye kurejea kuwa mkufunzi katika klabu kubwa.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Buffon achukua nafasi ya Neuer kikosi bora cha Fifa.
PESA YA KUMKUTANISHA NAY WA MITEGO NA YOUNGKILLER YAANZA KUNUKIA, VIPI KUHUSU ‘TRUE BOYA’ JUKWAANI?

Related articles

Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi…
Roma yaichapa Barcelona, Yatinga nusu…
Atlanta: Bodigadi wa Mayweather apigwa…
Je Mancity watafanikiwa ‘kuuwasha moto’…
Michael Carrick atangaza kutundika daluga…
Simba SC yatoa silaha zake…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise