HUKUMU YA ELIZABETH ‘LULU’ MICHAEL NI NOVEMBER 13.
Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo imetaja tarehe ya hukumu ya kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili staa wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael. Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua Steven Kanumba bila kukusudia, April 2012.
Hukumu hiyo sasa itatolewa November 13. Hatua hiyo imekuja baada ya wazee wa baraza la mahakama hiyo kutoa maoni yao mahakamani hapo ambapo wote watatu wamesema Lulu alimuua Kanumba bila kukusudia.
Kesi hiyo imesikilizwa kwa siku 5 mfululizo.