
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai ya kutokupokea simu za…
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani TABORA limekanusha madai ya wakazi wa mjini TABORA kwamba halipokei simu za taarifa za matukio, kuchelewa kufika kwenye matukio na kuwa na idadi ndogo ya askari.
Kamanda wa kikosi cha Zimamoto na Ukoaji mkoani TABORA,KONDO MOHAMED amesema madai hayo siyo sahihi na kwamba kikosi chake kipo makini na kinafanya kazi zake kwa taratibu zilizopo kisheria.
Ameeleza kuwa madai yanayotolewa na wakazi wa mjini hapa hayana kweli kwa sababu kikosi chake kinapokea simu za matukio,kuwahi kwenye matukio yote na kinakwenda katika matukio hayo kikiwa na idadi ya askari waliopo kituoni kwa kila siku husika.
KONDO amesema kuwa kwa wastani wanapokea simu 50 za matukio kwa siku,wanawahi kwenda katika matukio yote na kwamba kwenye matukio yote kinachotakiwa ni ufanisi wa utendaji kazi na siyo idadi idadi ya askari wanaotendakazi katika matukio hayo.
Pia amesema changamoto zinazowakabili katika utendajikazi ni wananachi wasio waaminifu kutoa taarifa za uongo za matukio na miundo mbinu mibovu ya ujenzi wa majengo usiofuata taratibu za mipango miji.