
KIGOMA: Upungufu wa Madaktari katika hospitali ya rufaa ya…
Upungufu wa madaktari bingwa na baadhi ya vipimo muhimu ikiwemo mashine ya CT Scan katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa KIGOMA -MAWENI unasababisha wagonjwa wengi kuingia gharama za kufuata huduma hizo katika hospitali nyingine za rufaa.
Hali hiyo imechangia hospitali hiyo kutoa rufaa kwa wagonjwa kati ya 40 hadi 50 kwa mwezi ili wapate huduma katika hospitali za BUGANDO, MUHIMBILI na KCMC MOSHI, jambo linalochangia wagonjwa wengi kushindwa kumudu gharama hizo huku hospitali ikiingia gharama za kuwasafirisha wagonjwa wakiwa mahututi.
Kwa mujibu wa mganga mkuu wa mkoa wa KIGOMA,Daktari PAUL CHAWOTE a hospitali ya MAWENI ina madaktari bingwa wawili tu kati ya 21 wanaohitajika.
Pia amesema watumishi wengine wanahitajika ili kupunguza tatizo katika vituo vya afya na zahanati hasa maeneo ya vijijini.