Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Kisutu: Mahakama haina mamlaka kuondoa mashtaka yanayomkabili Dk. Ringo…

  • November 24, 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema haina mamlaka ya kuyaondoa mashtaka ya utakatishaji fedha wa Dola za Kimarekani Milioni 3.7 katika kesi inayowakabili vigogo wa Kampuni ya mawasiliano ya Six Telecoms.

Vigogo hao ambao ni washatakiwa ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Wakili maarufu Ringo Tenga, Mhandisi Mkuu wa kampuni hiyo, Hafidhi Shamte , Mfanya biashara na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Peter Noni, Mkuu wa fedha wa kampuni hiyo, Noel Odeny Chacha na kampuni ya Six Telecoms Limited.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu , Victoria Nongwa ambapo amesema uamuzi huo unatokana na hoja za upande wa utetezi kuwa kuna baadhi ya mashtaka yana upungufu kisheria.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Victoria alisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kufanya lolote katika kesi hiyo hadi upelelezi utakapo kamilika au kibali kitakapo tolewa na DPP kuhusu kesi hiyo kusikilizwa hapo.

“Hivyo washatakiwa mtaendelea kubaki rumande hadi upelelezi utakapo kamilika naahirisha kesi hadi Disemba 12 mwaka huu.”

Washtakiwa hao wanadaiwa kuisababishia TCRA hasara ya USD 3,736,861 sawa na Tsh. Bilioni 8.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

TABORA: Wanafunzi WANNE wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari IKOMWA wahindwa kuendelea na masomo baada ya kugundulika kuwa ni wajawazito.
Janet Jackson na Jermaine Dupri waanza kunyemeleana upya

Related articles

Msanii Sam wa Ukweli ameaga…
Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise