Ligi daraja la kwanza TANZANIA BARA itaendelea Jumamosi na…
Ligi daraja la kwanza TANZANIA BARA itaendelea Jumamosi na Jumapili wiki hii kwa michezo sita.
Kwa kundi A kinara wa kundi hilo JKT RUVU itacheza na KILUVYA UNITED ya PWANI,ASHANTI UNITED na FRIEND RANGERS zote za DAR ES SALAAM.
Katika kundi B MUFINDI ya IRINGA itacheza na JKT MLALE ya SONGEA Na timu ya KMC ya DAR ES SALAAM dhidi ya COASTAL UNION ya TANGA.
Katika uwanja wa ALI HASSAN MWINYI Mjini TABORA wenyeji RHINO RANGERS watapambana na JKT OLJORO ya ARUSHA ikiwa ni mchezo wa kundi C wakati TOTO AFRICA ya MWANZA itawaalika TRANSIT ya SHINYANGA katika uwanja wa CCM KIRUMBA.