Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Lionel Messi awafikisha Argentina Kombe la Dunia 2018 Urusi.

  • October 11, 2017
Messi akishangalia baada ya kufunga goli, jana Leonel Messi aliisaidia Argentina kwa kufunga magoli matatu (hat-trick).

Lionel Messi alifunga mabao matatu na kuiwezesha Argentina kutoka nyuma ugenini dhidi ya Ecuador na kuwalaza 3-1 na kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Brazil walikuwa tayari wamefuzu.

Luis Suarez alifunga mabao mawili kuwawezesha Uruguay kulaza Bolivia 4-2 na kufuzu pia.

Colombia pia wamesonga mbele baada ya kutoka sare 1-1 ugenini Peru.

Peru walimaliza wa tano katika michuano ya kufuzu Amerika Kusini na sasa watakutana na New Zealand katika mechi mbili za muondoano za kufuzu.

Lakini nyota wa Arsenal Alexis Sanchez na taifa lake la Chile wako nje ya michuano hiyo baada ya kushindwa 3-0 ugenini Brazil.

Argentina walianza siku wakiwa nambari sita na kwenye hatari ya kutofuzu kwa mara ya kwanza tangu 1970.

Aidha, walianza vibaya katika mechi hiyo iliyochezewa mji ulio nyanda za juu wa Quito. Wenyeji walijiweka kifua mbele baada ya sekunde 38 kupitia bao la Romario Ibarra, bao la kasi zaidi ambalo Argentina wamewahi kufungwa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

Hata hivyo, Argentina, waliomaliza wa pili Kombe la Dunia nchini Brazil 2014, walijikwamua wakisaidiwa sana na ustadi wa Messi.

Alisawazisha baada ya dakika 12 aliposhirikiana vyema na nyota wa zamani wa Manchester United Angel di Maria.

Bao lake la pili alilipata dakika nane baadaye na kisha akafunga la tatu na la ushindi kipindi cha pili.

Alexis Sanchez.

Chile, ambao wameshinda Copa America katika michuano miwili ya karibuni zaidi, walikuwa wanapigania kufuzu kwa mara yao ya tatu mtawalia baada ya kufuzu na kufika hatua ya 16 bora mwaka 2010 na 2014.

Walianza mechi za mwisho wakiwa nafasi ya tatu lakini walifungwa mabao mawili na Brazil katika kipindi cha dakika tatu kipindi cha pili kutoka kwa Paulinho na Gabriel Jesus.

Baada ya Peru kufunga bao la dakika ya mwisho la kusawazisha dhidi ya Colombia, Chile walihitaji kufunga kujipatia nafasi ya kucheza mechi za muondoano za kufuzu.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Wazazi na walezi wenye watoto wanaogua saratani wametakiwa kuwafikisha mapema katika vituo vya tiba ili wapate matibabu kwa wakati.
Ndege za kivita za Marekani zapaa rasi ya Korea

Related articles

Simba Yamsajili Adam Salamba.
Roman Abrahamovich ahamia Israel.
Kipa wa Liverpool atishiwa maisha.
Haji Manara, Simba na Yanga…
Serengeti Boys wa Tanzania watwaa…
Wachezaji wanajua umuhimu wa mechi…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise