Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
Entertainment

Lupita Nyong’o kuchapisha kitabu cha watoto.

  • January 18, 2018

Mshindi wa tuzo ya Academy Lupita Nyong’o, atachapisha kitabu chake cha kwanza kuhusu watoto ”Sulwe” akishirikiana na wachapishaji wa vitabu vya Simon na Schuster kwa wasomaji wadogo Januari.

Sulwe ikimaanisha ‘nyota’ kwa lugha ya Kiluo ni hadithi ya mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitano ambaye amelelewa nchini kenya.

Katika kitabu hicho , Sulwe ni msichana mweusi katika familia yake, swala linalomfanya kuwa na wasiwasi na sasa ameamua kutafuta njia ya kung’arisha ngozi yake na kuwa mweupe.

Huku habari hiyo ikiendelea, Sulwe anaanza safari ambayo kupitia ushauri wa mamake inamsaidia kuelewa urembo kwa njia tofauti.

Kwa Bi Nyongo, uamuzi wa kugusa ama kuzungumzia kuhusu mada hii nzito katika kitabu cha watoto ulikuwa wazi.

Hadithi hiyo inapanda mbegu katika akili ya wototo , hatua inayoruhusu watoto kupata mafunzo ambayo hawayatambui wakati wanaposoma vitabu, alisema bi Nyongo katika mahojiano.

Wakati anapofikiria kuhusu safari yake ya kuikubali nafsi yake na kujipenda, bi Nyong’o anasema kuwa hatua yake ya kusoma na mamake ilimsaidia sana katika ukuwaji wake.

Kama Sulwe, Bi Nyongo aliyeigiza katika filamu za “Star Wars: The Force Awakens alijitahidi na rangi yake katika utoto wake.Alikumbuka kujitambua katika shule ya upili na kujali kuhusu maono ya watu wengine.

Ni wakati huo ambapo aligundua lugha inayotumiwa na watu wa nje ya familia yake kuelezea rangi ya ngozi ya dadake waliodai kuwa ”nzuri”.

Bi Nyongo alitambua kuwa na wasiwasi kuhusu ngozi yake katika hotuba isioweza kusameheka 2014.

Baadaye alitumia tamko lake kuwasilisha ujumbe mkali kuhusu umuhimu wa rangi na uwakilishaji katika Hollywood na kwengineko.

Pia alizungumza na shabiki wake kijana ambaye aliamua kutojichubua ili kuwa na rangi ya kung’ara baada ya kushuhudia ufanisi wa Bi Nyongo kama mwigizaji.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Uingereza yamteua waziri wa upweke
Wakimbia Kijiji baada kushindwa kutoa ufafanuzi wa michango ya wananchi.

Related articles

Mashabiki wa klabu ya YANGA…
Lagos, NIGERIA: Yemi Alade na…
STEPH CURRY aiongoza Golden State…
ShiiKANE Diamond alistahili tuzo
The Story of Adisson yaharibu…
Nicki Minaj kuachia albamu yake…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise