Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Maelfu wakimbia vita Jamhuri ya Afrika ya Kati

  • December 13, 2017

Zaidi ya watu 10,000 wamekimbia mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati. Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu milioni moja wameyama makazi yao nchini humo na wengine milioni 2.4 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Zaidi ya watu 10,000 wamekimbia mapigano Jamhuri ya Afrika ya Kati, hiyo ikiwa ni kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Msalaba Mwekundu.

Msemaji wa shirika hilo Sylivie Pellet amesema hatua hiyo inafuatia mapigano yaliyoibuka mwezi uliopita yakihusisha makundi kadhaa yaliyo na silaha karibu na mpaka wa nchi hiyo na Chad.

Pellet amesema maelfu ya watu wanaripotiwa kuuawa katika eneo la mpaka kaskazini mwa nchi hiyo. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Novemba lilikubali kurefusha muda wa wanajeshi wa kulinda amani nchini humo kwa mwaka mmoja zaidi na kuahidi kuongeza wanajeshi 900 ili kuzuia machafuko nchini humo.

Umoja wa Mataifa unakadiria zaidi ya watu milioni moja wameyama makazi yao nchini humo na wengine milioni 2.4 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Zaidi ya watoto laki nne wapo hatarini kutokana na utapiamlo DRC
TABORA: Agizo la Rais Daktari JOHN POMBE MAGUFULI kuhusu wasanii wa kike kuvaa nguo za heshima laanza kufanyiwa kazi.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise