Maneno ya Mkwasa kwa Mashabiki.
Uongozi wa Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania ,Yanga umewaomba mashabiki wa Soka kuhakikisha wanakata tiketi mapema ili kuepukana na usumbufu utakaojitokeza na fujo ambazo hazina tija wakati wa mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga Jumamosi wiki hii.
Katibu Mkuu wa Yanga Boniface Mkwasa ametoa rai hiyo kwa mashabiki wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kuwa Uwanja wa Uhuru unauwezo wa kuingiza mashabiki elfu ishirini na mbili pekee, hivyo kuna wasi wasi mkubwa wa mashabiki kushindwa kuingia kwa kiwango kikubwa.
Akizungumzia mchezo huo na maandalizi ya timu yao ya Yanga Afisa habari wa Yanga Dismas Ten amesema kikosi hicho kwa saa kipo kambini Morogoro kikijifua kwa ajili ya mchezo huo na ameeleza kuwa wachezaji waliokuwa majeruhi Donald Ngoma, Thaban Kamsoko pamoja na Amis Tambwe wamerejea katikahali zao na kuanza mazoezi.
Simba, Yanga pamoja na Mtibwa Sugar zote zinalingana kwa pointi hivi sasa, kila moja ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza