
Mhe. Tundu Lissu awatoa hofu Watanzania
Mbunge wa Singida Mashariki, Mhe. Tundu Lissu amewatoa hofu Watanzania juu ya afya yake kwa kusema kuwa hali yake inaendelea kuimarika.
Akielezea hali yake, Mhe. Tundu Lissu amesema kwa sasa anauwezo wa kukaa bila kuegemea kwenye kitu chochote, hali ambayo awali alikuwa anashindwa kufanya hivyo.
“Ninawashukuru kwa sala na maombi yenu. Sasa ninaweza kukaa bila ya kuegemea kitu.“ameandika Mhe. Lissu kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Juzi Jumanne Desemba 26, 2017 Mhe. Lissu alisimama kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Madaktari baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana mnamo mwezi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.