Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise

Mhubiri aliyetabiri kuwa Mugabe angefariki tarehe 17 mwezi huu…

  • October 19, 2017
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe.

Mhubiri ambaye alitabiri kuwa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe angefariki siku ya Jumanne, kwa sasa anajaribu kujitetea kwa sababu utabiri wake haukutimia, akisema kuwa Mungu amebadilisha fikra zake.

“Sababu iliyosababisha Mungu kuhairisha hili, hakuniambia – kwa hivyo sijui ni kwa nini Mungu aliamua kuchukua mkondo huo. Ninajua watu wengi walikuwa wakitarajia kutimia kwa unabii kwa sababu ya kile kinachoendelea nchini mwetu.”

Mhubiri huyo raia wa Zimbabwe Philip Mugadza alijaribu kuishawishi mahakama ya juu nchini humo kutupa kesi dhidi yake kwa kutabiri kuwa Rais Robert Mugabe, 93, angefariki tarehe 17 mwezi Oktoba mwaka 2017.

Kesi hiyo itarudi mahakamani ambapo mhubiii Mugadza – kiongozi wa kanisa la The Remnant ameshtakiwa.

Wakati wa kukamatwa kwake wakili wake Gift Mtisi aliiambia BBC kuwa “anakubali kusema hivyo. Anasema hakudanganya – huo ni ujumbe kutoka kwa Mungu. Polisi watahitaji kuthibitisha kuwa Mungu hakusema hilo.”

Mawakiia wake pia waliitaka mahaka ya katiba kutupilia mbali mashtaka hayo kwa misingi kuwa yanakiuka haki yake ya uhuru wa kusema.

Mwendesha mashtaka anasema kuwa muhubiri huyo alitukana dini ya kikiristo na tamaduni za Afrika kwa kutabiri kifo cha Mugabe.

Kutabiri kifo cha kiongozi ni mwiko, kulingana na imani za kitamaduni.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Ugonjwa wa shinikizo la jicho wazidi kushika kasi TABORA.
Uchaguzi Kenya: Mkuu wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati akutana na Raila Odinga

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise