Milambo FC tunaelekeza nguvu zetu katika ligi daraja la…

Baada ya kutoka sare tasa na wekundu wa msimbazi SIMBA katika mchezo wa kirafiki,klabu ya soka ya MILAMBO FC ya mkoani TABORA imesema kwa sasa inaelekeza nguvu zake katika mashindano ya ligi daraja la pili.
Kocha mkuu wa MILAMBO,ANDREW ZOMA amesema kwa wiki moja iliyobaki atahakikisha anayafanyia kazi makosa madogomadogo aliyoyaona katika mchezo wa jana.
Kwa upande wake msemaji wa klabu ya SIMBA HAJI MANARA amewataka wana TABORA kuipa ushirikiano MILAMBO ili ipande ligi daraja la kwanza na badae ligi kuu. SIMBA na MILAMBO wamecheza mchezo huo kwa lengo la kuviandaa vikosi vyao katika ligi wanazoshiriki.