
Milioni 334 zatengwa kwa ajili kuzigawa kwenye vikundi vya…
Jumla ya shilingi milioni 334 zimetengwa na Halmashauri ya wilaya ya KALIUA kwa ajili ya kuzigawa kwenye vikundi vya wanawake wa vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari,mbunge wa jimbo la KALIUA,MAGDALENA SAKAYA amesema kutokana na utoaji wa fedha hizo umeonyesha matokeo chanya kwa wanawake na vijana wilayani humo.
Amesema kwa sasa halmashauri ya wilaya ya KALIUA imeweka imetoa kipaumbele kwa mikopo kwa ajili ya wanawake na vijana ili kuwakopesha na waowaweze kushughulika na uzalishaji mali.
Katika kikao cha 30 cha mkutano wa 11 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA,mbunge wa viti maalumu kupitia CCM,SIKUDHAN CHIKAMBO ametaka kujua serikali inafanya nini kuziwezesha halmashauri nchini kuweza kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa wanawake na vijana.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI-GEORGE KAKUNDA amesema kuwa serikali imetoa maelekezo kwa halmashauri zote nchini kuhakikiha inafanya mapitio katika vyanzo vyake vya mapato.
Halmashauri zote nchini zinatakiwa kutoa asilimia kumi kwa ajili ya wanawake, vijana na wenye ulemavu.