Mkuu wa mkoa wa TABORA bwana AGGREY MWANRI ametaka…

Mkuu wa mkoa wa TABORA,Bwana AGGREY MWANRI ameagiza watumishi wote wa halmashauri ya wilaya ya UYUI walioshindwa kutekeleza mradi wa usimamizi endelevu wa Miombo wa ujenzi wa mabanda ya kuku na majiko sanifu wilayani humo wachukuliwe hatua.
Watumishi hao ni Afisa Kilimo,HUMPREY KIRUA,Mratibu wa Usimamizi Endelevu wa Misitu ya MIOMBO wilayani UYUI,Bwana CLISPO KISOMA,Afisa Ushirika RASHID MPUYA,Afisa Nyuki JONAS NTABAGI,Afisa Mifugo VICENT CHACHA, Afisa Maendeleo ya Jamii,ROBERT MIGANGWE na Afisa Ardhi,IBRAHIM MRAGANA.
Mratibu wa mradi wa MIOMBO mkoa wa TABORA,Bwana JOB KIUNGO amesema fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi imeshatumwa,lakini halmashauri haijazitumia fedha hizo.