Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
Local

Msanii Sam wa Ukweli ameaga Dunia.

  • June 7, 2018

Msanii wa Bongo Fleva, Salum Mohamed aliyetamba kwa jina la Jukwaani kama Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2018.

Sam alitamba sana na kazi zake kama vile Sina Raha alioutoa katika ya mwaka 2009 na 2010, Usiniache, Lonely na Hata kwetu wapo.

Hapo kati kati alipotea mpaka mwishoni mwa mwaka 2017 alipoibuka na kibao kingine kwa jina Kisiki na baadaye mwanzoni mwaka huu wa 2018 akauachia Wimbo Ni Wewe.

Ingawa ni mtu wa Singida Sam wa Ukweli amekulia Kiwangwa jirani na mji wa Dar es Salaam ambako amelelewa na Bibi yake mzaa mama.

Kwa mujibu wa aliyekuwa Meneja wa msanii huyo, Abdulmalik Mohamed , mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na mipango ya mazishi inaendelea katika eneo la Ilala lakini Maziko yatafanyika Alhamis hii Kiwangwa mkoani Pwani.

Aidha meneja huyo amesema chanzo cha kifo cha msanii huyo ni Malaria na UTI (Urinary Tract Infection) ya muda mrefu.

Sam alikuwa akiandaa nyimbo zake mpya kabla ya kuanza kusumbuliwa na Tumbo akiwa Studio.

Ameacha mke na mtoto mmoja wa kike.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa Kusimamia kombe la dunia ‘anaswa’ kwa rushwa.
Mabaki ya ndege iliotoweka na abiria 10 nchini Kenya yapatikana

Related articles

Mazishi ya pacha Maria na…
Vladmir Putin aizuru Austria.
Jeshi la Zimamoto lakanusha madai…
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri…
Serikali imetenga fedha kwa ajili…
Serikali kuwalipa fidia wananchi wa…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise