Mtu mmoja amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni…
Mtu mmoja amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni katika wilaya ya URAMBO mkoani TABORA.
Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi WILBROAD MUTAFUNGWA amesema tukio hilo lilitokea usiku wa Jumatano wiki hii.
Katika tukio jingine Kamanda MUTAFUNGWA amesema jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa 11 wa matukio mbali mbali mbali ya uhalifu yakiwemo ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake pia amesema watu wasiojulikana wamesalimisha bunduki SABA na magazine moja katika kijiji MWAMALUGU, kata ya KILUMBI wilayani SIKONGE.
Kamanda wa polisi mkoa wa TABORA amesema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika mkoa imeendelea kuimarika kutokana na jitihada za jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kupambana na vitendo vya uhalifu.