Nelly adaiwa kubaka katika tamasha la muziki

Msanii wa muziki nchini Marekani Nelly amedaiwa kumbaka mrembo wa miaka 21 katika mji wa Seattle bila kutumia kinga.
Nelly ambaye amewahi kushinda tuzo ya Grammy, alikutwa na sekeseke hilo siku ya Jumamosi na kupelekea kukamatwa na polisi ikiwa ni masaa machache baada ya kumaliza show yake maeneo ya King County.
Kufuati tukio hilo polisi wa Auburn, walimkiamata msanii huyo ambaye alikuwa katika gari linalodaiwa kutenda kosa hilo na kisha baadae walimuachilia.

Hata hivyo mwanasheria wa msanii huyo Scott Rosenblum, amedai kuwa msichana huyo anayedai kubakwa na mteja wake ni muongo na atapeleka ushaidi wote ikiwemo kufichua tabia za msichana huyo anazofanya kujipatia pesa.
Nelly ametumia ukurasa wa Twitter kuomba radhi mashabiki zake na kukanusha tukio hilo la ubakaji linalodaiwa kufanyika siku ya Jumamosi wikiendi iliyopita.