Nyota Ndogo aahidi kueleza A-Z yanayomtesa kwa miaka 17.

Muimbaji wa Kenya, Mwanaisha Abdallah maarufu kama Nyota Ndogo amekuwa akiwaacha mashabiki wake na maswali mengi kwa kulalamika muda mwingi kupitia mitandao yake ya kijamii kuwa kuna baadhi ya vitu vimekuwa vikimtesa kwa takribani miaka 17 sasa.
Je unataka kujua ni vitu gani hivyo ambavyo vimekuwa vikimsumbua mrembo huyo kwa muda wote huo? Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo ameahidi kufunguka kila kitu kwa kuweka wazi Jumatano hii.