Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Rais Mnangagwa: Nitampa mafao mazuri Robert Mugabe

  • January 25, 2018

Rais mpya wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, ameiambia BBC kuwa, atampa malipo mazuri ya kustaafu Rais aliyeng`olewa mamlakani Robert Mugabe na mkewe.

Amesema kuwa Mugabe ataendelea kupokea mshahara wake na mafao mengine kama kawaida ikiwemo kusafiri katika kiwango cha kwanza kwenye ndege (first class), pamoja na kusafiri kwa gharama ya serikali.

Lakini Rais Mnangagwa amesema kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na asiyeweza kushtakiwa.

Na Amesema kuwa Zimbabwe itajiunga tena hivi kariubuni na mataifa ya jumuia ya madola.

‘Hatujampa kinga mtu yoyote isipokua ambacho nimeahidi kwa rais aliyetangulia na baba wa taifa letu, rais Robert Mugabe ni kwamba tunampatia mafao na mshahara wake kama alivyokua akipata awali, usafiri, ofisi, ulinzi, na serikali yangu itamuwezesha kuenda Singapore kwenye matibabu, na vyote hivi mke wake pia ataviapata”.

Mnangagwa amesema pia serikali yake mpya inafanya jitahada kubwa za kupambana na rushwa.

” Msimamo wangu ni kwamba Rushwa haiwezi kuvumiliwa hata kidogo, hatuwezi kabisa kuvumilia jambo kama hili , na kama mnafatilia mambo yanayotokea Zimbabwe kwa sasa , watu wengi wenye wadhifa mkubwa wamefikishwa mbele ya mahakama, na ni ndani ya miezi miwili tuu tayari tunawashughulikia watu wenye makossa ya rushwa”.

Chanzo: BBC Swahili

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Daktari wa timu ya Olimpiki Marekani ahukumiwa kifungo
Watanzania 9 kusimamia mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise