Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Rais Trump aishutumu China kwa kukiuka vikwazo vya UN…

  • December 29, 2017

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa amevunjwa moyo na China kufuatia ripoti kwamba iliruhusu mafuta kusafirishwa hadi nchini Korea Kaskazini.

Katika Ujumbe wa twitter, bwana Trump alisema kuwa China ilionekana ”hadharani” ikiruhusu mafuta hayo kwenda Korea Kaskazini.

Amesema hakuwezi kuwa na suluhu ya kirafiki katika mgogoro wa Korea Kaskazini iwapo mafuta yataruhusiwa kusafirishwa hadi Pyongyang.

China mapema ilikana kwamba kumekuwa na ukiukaji wowote wa azimio la Umoja wa mataifa la mafuta kati ya China na Korea Kaskazini.

Wiki iliopita , Beijing iliunga mkono azimio la Umoja wa Mataifa lililoandikwa na Marekani ambalo lilishirikisha hatua za kupunguza kiwango cha mafuta kinacheolekea Korea Kaskazini kwa asilimia 90.

Vikwazo hivyo vikali ni jaribio jipya kuzuia majaribio ya silaha yanyotekelezwa na Pyongyang.

Matamshi hayo ya rais Trump dhidi ya China yanajiri baada ya gazeti moja la Korea Kusini Chosun IIbo kuripoti kwamba meli za China zimekuwa zikisafirisha mafuta kwa siri kupitia baharini kuelekea Korea Kaskazini.

Likiwanukuu maafisa wa serikali ya Korea Kusini, limesema kuwa usafirishaji huo unaenda kinyume na sheria kutoka meli moja hadi nyingine ulipigwa picha na Satellite za Marekani za ujasusi takriban mara 30 tangu mwezi Oktoba.

Maafisa wa Marekani hawakuthibitisha ripoti hiyo lakini afisa ya idara moja ya serikali aliyenukuliwa na reuters alisema kuwa usafirishaji huo huenda unaendelea.

Usafrishaji wa mafuta kutoka meli moja hadi nyingine unaendelea kuleta wasiwasi ikiwa miongoni mwa njia za Korea Kaskazini kukwepa vikwazo hivyo.

China ambayo ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa taifa la Korea Kaskazini , imesema kuwa inatekeleza vikwazo vyote vilivyowekwa na UN dhidi ya Korea Kaskazini.

Alipoulizwa maswali kuhusu ripoti za usafirishaji wa mafuta kutoka meli moja hadi nyingine, msemaji wa wizara ya ulinzi nchini China Ren Guoqiang aliambia maripota kwamba: hali ulioitaja haipo.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani Michael Cavey alisisitiza kuhusu wito wa mataifa yote kusitisha uhusiano wa kiuchumi na Korea Kaskazini.

”Tunatoa wito kwa China kusitisha uhusiano wowote wa kiuchumi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Korea Kaskazini ikiwemo utalii pamoja na uuzaji wa mafuta ama bidhaa za mafuta”, alisema.

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

George Weah achaguliwa kuwa Rais wa Liberia
Mhe. Tundu Lissu awatoa hofu Watanzania

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise