Serikali haitawavumilia wenye viwanda wanaotumia nguvu za fedha kuharibu…
Serikali imesema haitawavumilia wenye viwanda wanaotumia nguvu za fedha kuharibu mazingira.
Kauli hiyo imetolewa bungeni mjini DODOMA na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano na Mazingira KANGI LUGOLA akisema hatua hiyo ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Alikua akijibu swali la mbunge wa viti maalum mkoa wa TANGA, AMINA MOLENI aliyetaka kujua namna serikali itakavyodhibiti ujenzi wa viwanda usiathiri mabadiliko ya tabia ya nchi.