
TABORA: Biashara ya Magimbi yashamiri sokoni Kachoma
Biashara ya zao la magimbi maarufu kama mahole imeshamiri katika soko la KACHOMA mjini TABORA hasa katika mwezi huu Mtukufu wa RAMADHAN.
Akizungumza na CG FM,mmoja wa wafanyabiashara wa zao hilo KHALFAN KABATA amesema kuwa magimbi yanapatikana kwa wingi kipindi hiki na wateja wananunua kwa ajili ya kuandaa futari.
Mafungu ya magimbi kwa sasa yanauzwa kati ya shilingi elfu moja hadi shilling elfu mbili.