TABORA: Serikali inaendelea na juhudi ya kuhakikisha tumbaku inanunuliwa.

Serikali imesema bado inaendelea na juhudi kuhakikisha tumbaku ya wakulima wa mkoa wa TABORA iliyobakia kwenye maghala inanunuliwa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu, KASSIMU MAJALIWA wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni mjini DODOMA ambapo amesema serikali inaendelea kuzungumza na makampuni ya ununuzi wa tumbaku na nchi mbalimbali ili kuhakikisha tumbaku yote iliyobakia inanunuliwa.
Alikua akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa TABORA,MUNDE TAMBWE aliyetaka tamko la serikali kuhusu kununua tumbaku ambayo bado iko kwenye maghala hali inayosababisha kero kubwa wakulima wa tumbakuĀ mkoani TABORA.