TABORA: Serikali wilayani UYUI itawachukulia hatua kali za kisheria…
Serikali wilayani UYUI itawachukulia hatua kali za kisheria vijana watakao bainika kuwapa mimba wanafunzi na kuwataka wazazi na walezi kuwatimizia mahitaji watoto wa kike.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu mkuu wa wilaya ya UYUI,Mwalimu QUEEN MLOZI wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha KASOMELA,kata ya MAGIRI akisema wazazi wabebe jukumu lao la kuwapa mahitaji watoto wa kike.
Kwa upande wao ,wazazi SHABANI ALLY,JULIAS MAGANGA na ANETH JUMA wamesema tatizo la wanafunzi kupewa mimba linatokana wakati mwingine na wazazi kushindwa kuwahudumia,jambo linalosababisha watoto wa kike kuwa na tamaa na hatimaye kupata mimba wakiwa katika umri mdogo.