
TABORA: Shirika lisilo la kiserikali la JSI limekabidhi vifaa…
Shirika lisilo la kiserikali la JSI limekabidhi vifaa kazi kwa jamii katika halmashauri ya manispaa ya TABORA kwa ajili ya kuwafikia watoto wanaishi kwenye mazingira hatarishi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo,Mkurugenzi wa shirika la JSI -kanda ya kati na kaskazini,ANTONI MWENDAMAKAamesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwapa wasimamizi waliojitolea kuwajibika na kuwafikia kwa urahisi watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Akipokea vifaa hivyo,Mkurugenzi wa manispaa ya TABORA,BOSCO NDUNGURU amelipongeza shirika la JSI kwa kutoa vifaa hivyo na kwa kutoa mafunzo ya jinsi ya kuwafikia walengwa.
Kwa upande wao baadhi ya wasimamizi wa vifaa hivyo katika kata za halmashauri ya manispaa ya TABORA,Mwalimu BLANDESI wa kata ya KAKOLA na Mwalimu JASHIA HAMISI wa kata ya IKOMWA amefurahi kukabidhiwa vifaa hivyo kwa sababu vitawasaidia kutekeleza majukumu yao na kuwa rahisi kuwafikia walengwa kwa wakati na kutatua matatizo yao.
Halmashauri ya manispaa ya TABORA imekabidhiwa kabati kumi na moja na baiskeli kumi na moja na shirika la JSI kanda ya kati na kaskazini yenye makao makuu yake mjini DODOMA.