TABORA: Visima vichimbwe Ili kutatua tatizo la maji Kata…
Tatizo la ukosefu wa maji katika kata ya NDEVELWA katika manispaa ya TABORA limetatuliwa kwenye kijiji cha ITULU na vitongoji vyake huku juhudi za kutatua tatizo hilo zikiendelea katika vijiji vingine viwili.
Diwani wa kata ya NDEVELWA,SELEMAN MAGANGA amesema kwa miaka mingi kata hiyo imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ukosefu wa maji,lakini kwa sasa wamepatikana wahisani ambao wanaendelea na zoezi la uchimbaji wa visima.
Amesema mhisani huyo ambaye ni Mchungaji TIMOTHY kutoka nchini MAREKANI amepeleka katani NDEVELWA wataalamu kutoka mkoani MOROGORO ambao kwa sasa wanaendelea na kutafuta maeneo yenye maji katika kata hiyo ili wachimbe visima.