
TABORA: Wakulima wa tumbaku wapata hasara, UYUI.
Wakulima wa tumbaku katika kijiji cha NSIMBO,wilaya ya UYUI mkoani TABORA wamepata hasara kubwa kutokana na mvua ya mawe iliyonyesha ikiwa imeambatana na upepo mkali kuharibu zao hilo.
Wakizungumzana CG FM,baadhi ya wakulima JUMA KULWA na ABDALAH KISIMBA wamesema mvua hiyo kipindi cha nyuma iliharibu zao la tumbaku huku wengine wakivuna chini ya kiwango tofauti na matarajio yao.
Wamesema wana mikopo ya taasisi za fedha huku wakitakiwa kulipa kwa wakati mikopo yao jambo ambalo wanapata wakati mgumu kwa wakulima wa zao hilo la tumbaku.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha msingi cha nsimbo ihali NKWABI MATEO amesema kuwa mvua hizo ziliharibu kwa wingi zao la tumbaku huku akiomba tasisi za kibenki kuandaa utaratibu kwa wakulima kuweza kulipa madeni yao kwa hawamu.
Amesema kuwa zao la tumbaku limepanda bei tofauti na kipindi cha nyuma ambapo bei yake haikuwa nzuri licha ya kuwa wakulima kuvuna tumbaku chache.
Amesema zaidi ya ekari kumi na nane za tumbaku ziliharibiwa na mvua iliyokuwa imeambatana na upepo mkali siku chache zilizopita.
MWANDISHI:STEPHANIA LAISON,CGFM