TABORA: Wananchi wahimizwa kujitokeza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria

Wananchi mkoani TABORA wamehimizwa kujitokeza katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria ili kupata elimu kuhusu sheria sambamba na kupata msaada wa kisheria.

Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu-PARALEGAL mkoa wa TABORA,HOSEA KAMCHAMPE amesema kupitia maadhimisho ya wiki ya sheria wananchi watafahamishwa juu ya sheria  mbalimbali.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria mkoani TABORA yanaendelea katika uwanja wa CHIPUKIZI ambapo kilele chake ni kesho katika viwanja vya Mahakama Kuu,Kanda ya TABORA