TABORA: Wauzaji wa dawa na wamiliki wa maduka ya…
Wauzaji wa dawa na wamiliki wa maduka ya dawa muhimu Mkoani TABORA wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu za kuuza dawa ili kuepukana na adhabu zisizo za lazima.
Akizungumza katika kumbi za mikutano za GEORGE’S na MUSOMA UTALII, Mratibu wa mafunzo ya watoa dawa na wamiliki wa maduka ya dawa muhimu Mfamasia wa Manispaa ya TABORA MAGANGA KASOGA amesema wametoa mafunzo hayo kwa lengo la kuwezesha sheria kufuatwa ipasavyo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wamesema mafunzo hayo yamewajenga na wanatarajia kubadilika katika shughuli zao.