
TABORA: Zao la Mpunga Lashuka Bei.
Zao la mpunga limeanza kuvunwa katika kijiji cha ULYANKULU na kuuzwa mjini Tabora kwa bei nafuu tofauti na ilivokua awali.
Akizungumza na CG FM,mmoja wa wafanyakazi SAID HAMIS kutoka kampuni ya SIZYA MILLS inayojihusisha na uuzaji wa mpunga,kukoboa na kuuweka katika madaraja mpunga mjini TABORA amesema sasa ni kipindi cha mavuno ya mpunga na bei ya mchele imeshuka.
Bei ya mpunga wa kwa sasa ni shilling elfu nane kwa debe moja wakati awali bei ilikuwa shillingI elfu kumi na nane kwa debe.