
TABORA:Mradi wa ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa wakaribia…
Mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi MAJENGO kata ya MAJENGO wilaya ya UYUI,umefikia asilimiaa 98 kukamilika.
Akizungumzia ujenzi wa mradi huo Afisa elimu kata ya MAJENGO, REVOCATUS NSIMBILA amesema unaambatana na ujenzi wa matundu ya vyoo na utengenezaji madawati.
Akikagua mradi huo Mbunge wa jimbo la TABORA KASKAZINI, ALMASI MAIGE amesema alijitahidi kuomba serikali fedha za mradi huo na kwamba utakamilika hivi karibuni.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi MAJENGO, KASTOLI TANGWA amesema kukamilika kwa madarasa hayo kutasaidia kupunguza wingi wa wanafunzi kusoma katika darasa moja.
Kwa upande wke Mwalimu ELIZABETH KAMATA amesema watapiga hatua kubwa kitaaluma kulingana na madarasa hayo kukamilika.
Nao wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo SELEMANI MUSSA na PILI SADIKI wamesema madarasa hayo yatawasaidia wadogo zao walio madarasa ya chini kusoma kwa vizuri.
Baada ya kukamilika ujenzi wa madarasa hayo matatu utaongeza idadi ya vyumba vya madarasa kutoka saba vya awali hadi kufikia kumi.