TANESCO mkoa wa TABORA yalalamikiwa kwa kushindwa kushiriki kikamilifu…

Shirika la umeme nchini-TANESCO mkoa wa TABORA limelalamikiwa kwa kushindwa kushiriki kikamilifu katika matibabu ya mtoto ABDULKARIM IBRAHIM aliyepigwa na shoti ya umeme katika mtaa wa MAJENGO,kata ya IPULI mjini TABORA.
Akizungumza na CGFM,Baba mzazi wa ABDULKARIM,IBRAHIM ABDALAH amesema tangu mtoto wake apigwe na shoti ya umeme tarehe 12 mwezi uliopita TANESCO haijashiriki ipasavyo hadi imefikia hatua ya mtoto huyo kupewa rufaa ya kwenda katiaka hospitali ya rufaa BUGANDO jijini MWANZA.
Awali CG FM ilitaka kufahamu mazingira ya mtoto ABDULKARIM alipigwa na shoti ya umeme ambapo baba yake mzazi anaeleza.
Kwa upande wake,Mratibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA,Kanda ya magharibi GENERAL KADUMA amesema serikali inapaswa kuona uchungu juu ya mtoto huyo.
CG FM imemtafuta Meneja wa TANESCO mkoa wa TABORA,Injinia MOHAMED ABDALLAH kuzungumzia suala la mtoto huyo,lakini alikataa kuzungumza kwa madai kwamba suala hilo lipo kwenye uongozi wa juu yaani Makao Makuu ya TANESCO DAR ES SALAAM.
Naye Katibu wa mbunge wa viti maalum-CHADEMA,KWANDU MPANDUJI amesema mbunge wa viti maalum,HAWA MWAIFUNGA amemsafirisha mtoto ADBULKARIM kwenda BUGANDO kwa matibabu zaidi.
Tarehe 12 mwezi uliopita mtoto ABDULKARIMU IBRAHIM alipigwa shoti ya umeme wakati akienda shuleni baada ya kukuta nguzo ya umeme imeanguka na kushika nyaya zikiwa na umeme hali iliyosababisha mtoto huyo kukatwa mkono wake wa kulia baada ya kubainika mkono huo hauwezi kufanya kazi tena.