
Tanzania yaongoza kwenye ripoti ya nchi za kuwekeza Afrika
Tanzania inaendelea kufanya vizuri kisera katika sekta ya viwanda na uwekezaji Afrika baada ya ripoti ya r&b investment index kuonyesha Tanzania imepanda nafasi mbili katika nchi zinazovutia kwa uwekezaji Afrika.
Amesema hayo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uwekezaji wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Aristide Mbwasi wakati wa uzinduzi wa kiwanda kutengeneza mita za Umeme, Baobao Energy Systems Tanzania (BEST) kilichopo eneo la mbezi juu Dar es salaam.