Skip to content
CGFM
  • Home
  • Listen Live
  • News
  • Presenters
  • Gallery
  • Advertise
International

Ujerumani yagundua akaunti bandia za Wachina

  • December 26, 2017

Shirika la Ujasusi la Ujerumani (BfV) limechapisha taarifa za watumiaji wa mitandao ya kijamii linaosema ni majina feki yanayotumiwa na majasusi wa Kichina kukusanya taarifa kuhusu maafisa na wanasiasa wa Ujerumani.

Shirika hilo la ujasusi wa ndani lilichukuwa hatua hiyo isiyo ya kawaida kwa kuwataja majina watumiaji wa mitandao ya kijamii na taasisi bandia ili kuwaonya maafisa wa serikali juu ya kitisho cha kupenyeza taarifa muhimu kupitia mitandao hiyo.

“Majasusi wa Kichina wako kwenye mitandao kama vile Linkedln na wamekuwa wakijaribu kwa kitambo kirefu sasa kukusanya taarifa na kupata vyanzo vya kijasusi kwa njia hii,” ikiwemo kusaka taarifa za tabia za watumiaji, mambo wanayopendelea na muamko wao kisiasa, linasema shirika hilo.

Miezi tisa ya utafiti wa shirika hilo umegundua kwamba zaidi ya raia 10,000 wa Kijerumani wamewahi kutafutwa kupitia mtandao wa wasomi wa Linkedln na akaunti bandia ambazo zinajitambulisha kama washauri, wataalamu, wabunifu ama wasomi, lilisema shirika la BfV.

“Inawezekana kuna idadi kubwa zaidi ya watu waliolengwa na akaunti bandia ambazo bado hazijatambuliwa,” kwa mujibu wa maafisa wa BfV.

“Tunatarajia taasisi sahihi za Kijerumani, hasa idara za serikali, zinaweza kusema na kutenda mambo kwa utaratibu na sio kufanya vitu ambavyo havina faida kwa maendeleo ya mahusiano kati ya pande hivi mbili,” alisema Lu.

Miongoni mwa akaunti bandia ambazo taarifa zake zilichapishwa na BfV, ni ya “Rachel Li” anayejitambulisha kama kiongozi wa taasisi ya RiseHR na “Alex Li” anayejitambulisha kama “Meneja Miradi kwenye Kituo cha Utafiti kati ya Ulaya na China.”

Nyingi kati ya akaunti hizo zina picha za vijana warembo wa kike na wa kiume. Picha ya “Laeticia Chen”, meneja kwenye “Kituo cha Siasa za Kimataifa na Uchumi” ilitolewa kutoka mtandao wa warembo, anasema afisa wa BfV.

Utafiti wa shirika la habari la Reuters kwa taarifa hiyo umegunduwa kuwa baadhi ya akauti hizo zimeunganishwa na wanadiplomasia wa ngazi za juu na wanasiasa kutoka mataifa kadhaa ya Ulaya. Hata hivyo, haikufahamika mara moja ikiwa pamewahi kufanyika mawasiliano baina yao.

Onyo hili la shirika la ujasusi la Ujerumani linaakisi wasiwasi unaoongezeka barani Ulaya na miongoni mwa mashirika ya kijasusi ya Magharibi juu ya harakati za chini kwa chini za China na pia linafuatia onyo kutoka Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) juu ya uwepo wa jitihada za kuwapa mafunzo raia wa Kimarekani kuyafanyia ujasusi mashirika ya Kichina.

BfV imewaalika watumiaji wa mitandao ya kijamii wenye wasiwasi kuwasiliana na shirika hilo endapo wameona akaunti zinazotiliwa mashaka.

Mwandishi: Mohammed Khelef/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Share this:

  • Click to share on Twitter (Opens in new window)
  • Click to share on Facebook (Opens in new window)
  • Click to share on Google+ (Opens in new window)

Related

Hasimu mkubwa wa Putin Alexei Navalny azuiwa kuwania urais
Leo ni duru ya pili ya uchaguzi wa urais Liberia kati ya George Weah na Joseph Boakai

Related articles

Mabaki ya ndege iliotoweka na…
Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa…
Rais Madagascar ateuwa waziri mkuu…
Bodi ya usimamizi wa shule…
Mchungaji auawa akiwabatiza waumini Ziwani
Volkano yasabisha vifo vya watu…

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

On Air Now

Download CG Google App here

CLICK TO PLAY CG ONLINE TV

Advertise here

ABOUT US

CG FM RADIO is the radio station that based in Tabora – Tanzania that targets all age groups. Due to its moral observation and ethical programs, CG FM radio continues to have a lot of audience which makes us the best on western zone.

YOU ARE HOME

TWITTER

My Tweets

Menu

  • HOME
  • News
  • Listen Live
  • Advertise