Vijana mjini TABORA wametakiwa kuachana na utamaduni wa kuvaa…

Vijana mjini TABORA wametakiwa kuachana na utamaduni wa kuvaa miwani bila ushauri wa kitaalam kwa sababu kufanya hivyo ni kuathiri afya ya macho.
Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Kanisa la MORAVIANI MILUMBANI,Daktari LAMECK KISULILA akisema vijana wengi wanapenda kuvaa miwani ya urembo lakini wanapaswa kuwa waangalifu na ubora wa miwani hiyo.
Amesema kwamba watu ambao wanatumia miwani iliyothibitishwa na daktari katika shughuli zao hiyo ni moja ya tiba na siyo kwamba dawa ya kuwatibu imekosekana.